>

BEKI WA ZAMANI EPL, SOL BAMBA AFARIKI

Beki wa zamani wa Leicester City, Leeds United na Cardiff City, Sol Bamba ambaye amepoteza maisha Agosti 31, 2024 akiwa na umri wa miaka 39.

Bamba raia wa Ivory Coast ambaye alikuwa kocha wa kocha wa klabu ya Adanaspor inayoshiriki Ligi Kuu ya TFF Nchini Uturuki amefariki baada ya kuugua ghafla.

Taarifa ya klabu hiyo imesema:+ “Mkurugenzi wetu wa ufundi Souleymane Bamba, ambaye aliugua kabla ya mechi yetu dhidi ya Manisa iliyochezwa jana, alipelekwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Manisa Celal Bayar na kwa bahati mbaya akapoteza maisha.

Bamba ambaye alianza makuzi yake ya soka kunako klabu ya PSG pia amewahi kuitumikia klabu ya Middlesbrough katika miaka yake 18 ya kusakata kabumbu akicheza jumla ya mechi 423