>

AUGUSTINE OKRAH AREJEA KWENYE TIMU YAKE YA AWALI BECHEM UNITED

Nyota wa zamani wa Simba Sc, Augustine Okrah amerejea kwenye timu yake ya awali Bechem United inayohiriki Ligi Kuu nchini Ghana kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuondoka Young Africans Sc.

Okrah alijiunga na Simba Sc msimu wa 2022/2023 akitokea Bechem United kabla ya kurejea Bechem United na baadaye akajiunga na Yanga Sc katika dirisha dogo la msimu wa 2023/24 kwa mkataba miaka miwili.

Hata hivyo nyota huyo raia wa Ghana lakini hakupata muda wa kutosha wa kucheza kutokana na changamoto ya majeraha yaliyokuwa yanamuandama hali iliyopelekea kutemwa na Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu bara.