AZIZ KI ATANGAZWA KUSALIA YANGA, AZIMA TETESI

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ametangaza kuwa ataendelea kusalia klabuni hapo kwa msimu ujao wa 2024/25 kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake.

Ikumbukwe kwamba Ki  ana tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2023/24 alipogotea kwenye mabao 21 ndani ya ligi akivunja rekodi ya msimu wa 2022/23 alipofunga mabao 9 yote kwa mguu wake wa kushoto.

Nyota huyo alifunga mabao 17 kwa mguu wa kushoto matatu kwa mguu wa kulia na alitupia bao moja kwa pigo la kichwa Uwanja wa Mkapa mchezo dhidi ya Tabora United.

Alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada ya timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Simba ya Tanzania iliyokuwa ikipewa nafasi ya kuinasa saini yake kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umegota mwisho.

Julai 10 2024 uongozi wa Yanga umetangaza kuwa Ki bado atabaki Jangwani licha ya timu nyingi kupambania kuipata saini yake.

Hivyo kubaki kwake ndani ya Yanga kazima tetesi zilizokuwa zikimhusisha na kuondoka Jangwani baada ya kusaini mkataba mpya unaotajwa kuwa ni miaka miwili.

Anaungana na Clatous Chama, Pacome, Prince Dube, Maxi Nzegeli kwenye kutimiza majukumu ndani ya kikosi cha Yanga.