KIUNGO MGUMU SIMBA IMEISHA

KIUNGO mgumu ndani ya Simba, Sadio Kanoute imeisha hiyo ndani ya timu hiyo baada ya kukutana na Thank You.

Ipo wazi kuwa Kanoute raia wa Mali ni kiungo ambaye alikuwa akifanya kazi kubwa ndani ya uwanja msimu wa 2023/24 kwenye eneo la ukabaji.

Sifa yake kubwa ni kutembeza mikato ya kimyakimya kwa wapinzani akiwa na rekodi ya kuwa nyota aliyeoonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union.

Ilikuwa ni msimu wa 2022/23 Uwanja wa Mkwakwani, alionyeshwa kadi mbili za njano jambo lililopelekea kuonyeshwa kadi nyekundu mazima.

Ukiweka kando hilo Kanoute alibadilishiwa majukumu kwenye mzunguko wa pili chini ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha kwa zama hizo ambapo alikuwa kwenye eneo la ushambuliaji.

Rasmi Julai 9 2024 raia huyo wa Mali wengi walikuwa wakipenda kumuita Putin amekutana na Thank You hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu wa 2024/25.